French Montana adai kuwa Ghetto Boys wa Uganda wanacheza zaidi ya Chris Brown
French Montana alikuwa nchini Uganda hivi karibuni akifanya makala na
video zake na huko anasema alikutana na vijana wanaocheza kuliko Chris
Brown.
Montana anayetokea Moroco anasema 'Nimesafiri mahali ambapo watu wanaishi tofauti na sisi, nataka kusambaza ujumbe hapa Marekani kuwa kuna watu wanaishi tofauti na wanahitaji msaada wetu, vipaji vya ukweli pia haviko hapa, watoto nilioenda kuwaona wanacheza zaidi ya Chris Brown na hawana tv".
Video ya French Monatana aliyofanya Uganda inatoka April 7.
No comments