Rick Ross kuwa chini ya uangalizi wa polisi kwa miaka mitano kesi ya utekaji

Rick Ross na mlinzi wake Nadrian Lateef James watakuwa chini na uangalizi mkali wa polisi kwa miaka mitano.

Adhabu hii imetolewa baada ya rapa Rick Ross na mlinzi wake kukubali dili hili na mwanasheria wa serikali aliyekuwa akiwashati kwenye kesi yao ya utekaji toka mwaka 2015.

Rick Ross na James waliwateka vijana wao wawili wa kazi na kuwatesa kwa zaidi ya saa sita kwenye nyumba ya Rick Ross iliyopo Fayetteville, Georgia huku mfanyakazi mmoja akidai alipigwa na bastola usoni zaidi ya mar moja.

Masharti ya adhabu hii, Rozay hataruhusiwa kuonana na wafanya kazi hio, kumiliki silaha ya moto, kushika au kutumia dawa za kulevya na pombe, atasachiwa muda wowote na ameamrishwa kuhudhuria darasa la kumudu hasira.

Ross alitoa album yake ya tisa 'Rather You Than Me' mwezi uliopita. 

No comments

Powered by Blogger.