Baada
ya kusambaza mtandaoni picha zinazomuonyesha Ben Pol akiwa nusu mtupu
na mng’ao wa mafuta, Mkali huyo wa muziki wa RnB, amefunguka kwa kusema
kuwa sasa amepata dili ya kuwa balozi wa mafuta ya kujipaka na kwa sasa
wapo kwenye hatua za mwisho za mazungumzo.
Ben Pol amesema kuwa baada ya picha kusambaa, kuna makampuni yamemfuata na kutaka kufanya naye biashara ya matangazo. . . .
“Hapa sasa hivi tunaongea kuhusu majukumu yangu kama balozi, nione nina
show ngapi katika hiyo event na mambo ya maslai inakuaje, nione
matangazo ya runinga na mabango na nijue amount ya kazi yote ilivyo ni
kiasi gani ninaweza kunufaika.Tukifikia muhafaka watu wataniona kwenye
mabango, nimekoleza mafuta nimeweka na logo za hiyo kampuni,” alisema @iamBenPol
No comments