Dogo
janja amesema anaweza kutajwa kwenye Jarida la Forbes under 30 iwapo
mpango wake wa kuzindua brand kwa ajili ya watoto utafanikiwa . .
Dogo
janja amedai kuwa mipango yake sio kuja na nguo kama ilivyozoeleka kwa
wasanii wengi bali yeye mipango yake ni kuja na vifaa vya watoto vya
michezo pamoja na magemu ambayo yatakuwa katika brand yake . . .
. "Brand ya Dogo janja itakuja lakini mimi sitakuja na Brand ya nguo,
Nitakuja na vifaa vya watoto vya michezo vya Dogo janja nitakuja na
magemu ya Dogo janja yani mimi biashara yangu itakuwa ina'deal na madogo
dogo madogo janja" alisema @Dogojanjatz . .
Hata hivyo Janjaro ameweka wazi kwanini biashara yake ita'deal na watoto wadogo tu na si watu wazima . . .
"Biashara na mtoto, ujue ukifanya biashara na mtu mzima haitamuhusisha
mtoto lakini ukifanya biashara na mtoto itamuhusisha mtu mzima" alieleza
. .
Dogojanja ameongeza kuwa yupo
katika maandalizi ya kusafili na atakaporudi kwenye mwezi wa sita
biashara hiyo itaingia sikoni rasmi
No comments