. . Baada ya kutajwa kwenye jarida la Forbes kama mjasiriamali wa kutazama, Jokate Mwegelo amefunguka kama aliwahi kuhisi kama kuna siku atakuwepo kwenye list ya Forbes . . Jokate amesema Kupitia kidoti wameweza kushawishi vijana kujiajili, wameona fursa na kuzitumia kwahiyo alitegemea kutajwa kwenye Jarida la Forbes . . . "Pengine nilitegemea ningeweza siku moja kutokea kwenye hiyo list kwasababu ukiangalia kati ya vijana ambao wameweza ku-inspire na ku- motivate vijana wenzao kuweza kutafuta njia mbalimbali za kujiingizia kipato kuwa wabunifu na fursa ambazo zipo na jinsi gani ya kuzikamatia na kujiongezea thamani. Lakini ukiachana na hilo pia jinsi gani ya kuweza kujiajili mwenyewe kwasababu sio kila mtu anaweza kuajiliwa pengine wale wanaoweza kumaliza chuo na hata wale ambao hawajafika chuo lakini kuona tu fursa ambazo zipo na jinsi gani ambavyo unaweza kuzikamatia nadhani tumeweza kwa kiasi kikubwa kupitia brand ya kidoti na kampeni mbalimbali kuweza kutoa mwangaza huo na kushawishi vijana wengi tu waweze kuangalia maisha yao kiutofauti na kujibunia miradi mbalimbali ya kukizi mahitaji yao ya kila siku na kuongezea taifa letu kipato" alieleza @jokatemwegelo . . Forbes ni jarida maarufu duniani ambalo hufuatilia maisha ya watu maarufu duniani na kutoa takwimu mbalimbali zikiwepo watu wanaoingiza pesa nyingi zaidi duniani, mastaa wanaoongoza kwa malipo ama wajasiriamali wa kutazamiwa.
No comments