Startimes kuonyesha kombe la dunia 2018
Shirikisho la soka Dunia FIFA limetoa haki ya
kurusha matangazo ya michuano ya fainali ya
kombe la Dunia yatakayofanyika Russia mwaka
2018 kwa Starstimes kwa nchi za kusini mwa
jangwa la SAHARA.
Meneja masoko wa Starstimes Felix Awino
amesema watajitahidi kurusha matangazo bora
ya fainali za kombe la dunia kwa wateja wao
kwa kiwango cha juu huku mkuu wa bishara wa
FIFA Philippe Le Floc’h akisema wanayofuraha
kufanya ushirika na STARSTIMES kwani utasaidia
kufikisha matangazo ya soka kwa mashabiki wegi
wa soka Barani Afrika.
Nchi 42 kusini mwa Jangwa La Sahara, zitapata
matangazo hayo kutoka Starstimes huku pia
wakihusika kuonyesha fainali mbalimbali za FIFA,
kama vile, fainali za kombe la dunia la FIFA la
vijana wenye umri chini ya miaka 17 na 20,
fainali za kombe la Dunia la soka ya
Ufukweni,fainali za kombe la shirikisho,fainali za
kombe la dunia kwa wanawake wenye umri chini
ya miaka 17 na 20 za mwaka 2018 na fainali
zenyewe za kombe dunia la FIFA nchini.
No comments