JE! WAJUA NI KWA NINI MPAKA LEO MALENGO YAKO HAYAJATIMIA?
moja yachangamoto
ambayo inawakabili watu wengi ni kwamba ni wazuri sana wa kusema kuliko kuchua
hatua, hapa nina maana ya kwamba kila mmoja anapenda kuona matarajio yake
yanatimia, hata hivyo kutokana na imani hiyo imepekelekea watu wengi sana
kubaki na maisha yale yale kila siku. Unajua ni kwanini? Basi nakusihi ufuatane
nami kwani nataka nikijuze siri ambayo watu wengi hawaijui juu ya upangaji wa
malengo.
Ipo hivi niliwahi
kufanya uchunguzi mdogo katika kazi yangu ya uhamasishaji mahali fulani, moja
ya maada ambayo nilikuwa naizungumzia siku hiyo ilikuwa inahusiana na jinsi
gani unavyoweza kutimiza malengo yako na
kila mmoja ilionekana kufurahia somo hilo. Kila mmoja wetu ambaye ulikuwepo siku
hiyo ilionekana dhairi anayo ndoto ambayo inasukuma kufikia kilele cha
mafanikio.
Ndipo nikachukua
jukumu la kutaka kujua kila mmmoja aliyekuwepo siku hiyo ni nini ambacho
anaadhamiria katika maisha yake? Kila mmoja alieleza kwa mapana kutoka na
dhamira inavyomsukuma kutoka nafsini kwake. Baada ya kumaliza zoezi hilo la
kujua kila mtu lengo lake, ndipo nikawataka watu hao hao waandike kuhusiana na
njia ya kutimiza ndoto hizo.
Moja ya maajabu
ambayo niliyaaona ni kwamaba watu wengi ni wazuri sana wa kusema nataka kuwa
mtu fulani lakini linapokuja suala la utekelezaji wa jambo hilo hapo ndipo
ukakasi hujitokeza unajua ni kwanini? Niligungundua ya kwamba watu wengi wana
ndoto lakini hawajui mbinu za kutekekeza, hata wale ambao wanajua ni wepesi
sana wa kukuta tama. Ndipo nikawambia ya kwamba kwa jambo lolote ambalo
unalitamani liwe kweli ni lazima ujue mbinu ya utekelezaji wa jambo hilo
hususani kwa kujifunza na ikiwezekana kulipa gharama lipa gharama kwa kuwa
hakuna maisha ya kimafanikio ambayo hayana gharama.
Pia ikubukwe ya
kwamba katika kujifunza hukohuko kuna changamoto zake, changamoto hizo hizo ndizo
ambazo huwafanya watu wachache waweze kuhimili mikiki ya jambo hilo, na hawa ni watu ambao
wamefanikiwa katika sayari hii. Hata hivyo kwa asilimia kubwa ambapo wengi wetu
ambao ndio tupo humo huwa hatupo tayari kuvumilia mikikimikiki ya changamato
ambazo mara nyingi hujitokeza katika mambo amabayo tuanayafanya.
Wengi wetu tupo
tayari kuhairisha mambo na kuleta visingizio
visivyokuwa na maana yeyote ile, kwa mfano unakutana na mtu anakwambia anataka
kufanya biashara fulani lakini changamoto yake kubwa ni mataji. Kimsingi ukichunguza changamoto hiyo
utagundua ya kwamba ni sababu yatima, nikiwa na maana ya kwamba huna haja ya
kuacha kufanya jambo fulani eti kwa sababu ambazo hazina msingi wowote.
Tuende mbele turudi
nyuma na kuyatafakari maisha ambayo tunayaishi leo hii, ni kwanini yapo vile
vile? Ni wakati wako muafaka ewe msomaji ambaye unasoma makala haya kuweza
kutafakari kwa umakini jambo hili japo kwa dakika chache na kuendelea
kutafakari juu ya maisha yako. Tafakari ni kwanini mapka leo hii hujatimiza
malengo yako? Kama umepata jibu zama tena katika halmashauri yako ya kichwa
tafakari tena je unahisi sababu ambazo umezipata ni za msingi au sio za msingi? Kama umekwisha pata majibu
inua macho yako mbiguni, tazama mbigu inavyong`ara kisha tafakari tena na uje
na majibu ya kina je unachukua hatua gani kwa hayo yote uliyowaza? Usinibe
majibu.
Mmmh, sawa labda
nisiendelee kuongea sana, maana naweza nikakupoteza kabisa ila cha msingi ni
kwamba tafakari hayo machache kisha uchukue hatua mathubuti za kiutendaji. Hata
hivyo nikazie kwa kusema ya kwamba mara zote ukiwa na malengo usiishie kusema
tu, bali onyesha njia sahihi za utekezaji. Kufanya hivi kutukupa mwelekeo tosha
kwa upande wako kwa kuonesha ni nini! Ambacho unatakiwa kuwa nacho? Na baada ya
muda gani!
Huenda bado ukawa
haujanielewa nazungumzia masuala ya uwezo wa utekelezaji wa jambo hilo. Maana
tunafahamu ya kwamba ili yaitwe mafanikio kuna njia ya kufikia mafanikio hayo
kwa mfano kujifunza kutoka kwenye vitabu, video, semina na watu wengine ambao
kiujumla wamekwisha fanikiwa. Nikakumbushe kwa mala nyingine kuwa ni lazima uwe
na picha kamili ya kule ambapo unataka kuelekea.
Nikushuru sana kwa
kusoma makala haya, lakini shukrani zangu zangu zitakuwa zimekamilika endapo
utachukua hatua kwa hayo ambayo umekwisha yasoma kwenye makala haya. Nikusihi
ya kwamba ulichojifunza mshirikishe mwenzako kama ambavyo mimi nmefanya kwako.
Ndimi; Afisa miapngo
Benson Chonya
Blogu;
dirayamafanikio.blogspot.com
Simu; 0757909942
No comments