Jeshi la Polisi Lajibu tuhuma za vyeti feki
Jeshi la Polisi nchini limekanusha taarifa
zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikiwahusisha askari wake kuwepo
katika majina ya vyeti feki na kusema taarifa hizo ni za uongo na wala
hazijatolewa na Jeshi hilo.
Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa
Jeshi la Polisi, ACP Advera Bulimba na kusema wanaendelea kumtafuta mtu
aliyesambaza taarifa hiyo kwa lengo la kupotosha umma ili hatua kali za kisheria
zichukuliwe dhidi yake na kuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama
hiyo.
"Jeshi la Polisi nchini, linaujulisha umma kwamba,
orodha ya majina ambayo yamekuwa yakisambazwa kwenye mitandao ya kijamii yakidai
kuwa ni majina ya askari wa jeshi la polisi wenye vyeti feki ni ya uongo na wala
taarifa hiyo haijatolewa na jeshi la polisi". Ilisema taarifa
hiyo
No comments