Mama aliyejifanya mwanaume ili afanye kazi mgodini Tanzania
Pili Hussein alitamani kujiimarisha kimaisha na
mawe ya thamani yanayosemekana kuwa nadra mara elfu mia moja kuliko almasi,
lakini kwa kuwa wanawake hawakuwa wanaruhusiwa kwenye migodi hiyo alivalia
mavazi kama mwanamume na kuwadanganya wafanyikazi wenzake kwa zaidi ya mwongo
mmoja.
Pili alilelewa katika familia kubwa mjini
Tanzania. Mtoto wa mchugaji ambaye aliyekuwa na mashamba makubwa, babake Pili
alikuwa na wake sita na alikuwa miongoni mwa watoto 38.
Licha ya hayo yote alilelewa vyema kwa njia
tofauti.
''Babangu alinichukulia kama mwanamume na
nilikuwa nikichunga mifugo yake, lakini sikuyapenda maisha hayo kabisa'',
alisema.
Hata ndoa yake haikuwa ya furaha, akiwa na umri
wa miaka 31 Pili aliikimbia ndoa yake iliyokumbwa na migogoro ya
kinyumbani.
Alipokuwa akitafuta ajira alijipata katika mji
mdogo wa Mererani, Tanzania, uliopo chini ya mlima mkuu wa Kilimanjaro.
Eneo hilo ni maarufu sana duniani kwa kuwa na
madini nadra ya rangi ya samawati ya tanzanite.
''Sikwenda shule , kwa hivyo sikuwa na mambo
mechi kuchagua,'' Pili alisema.
''Wanawake wahakuruhusiwa kwenye maeneo ya
migodi hiyo, nikajitosa kama mwanamume shupavu na mwenye nguvu. Nilichukua
suruali ndefu na kuzikata zikawa kama kaputula ili kufanana na mwanamume. Hivyo
ndivyo nilivyofanya.''
Ili kukamilisha mabadiliko yake , alibadilisha
pia jina lake.
''Niliitwa Uncle Hussein {akimaanisha mjomba
Hussein}, sikumwambia yoyote kuhusiana na jina langu halisi la Pili.
Hata leo ukija katika kambi hiyo utanitafuta
kwa jina hilo la Uncle Hussein.''
Kwenye migodi hiyo yenye joto ,uchafu mwingi na
wenye kina cha mita mia moja chini ya ardhi Pili angefanya kazi kwa saa 10-12
kwa siku , akilima na kuchunga akiwa na matumaini ya kupata mawe hayo ya thamani
kwenye mishipa ya mawe hayo ya grafiti.
''Ningeenda hadi mita 600 chini ya mgodi, mara
kwa mara nikiwa shupavu kuliko wanaume wengine.
Nilikuwa na nguvu nyingi na niliweza kufanya
kazi kama matarajio ya wanaume wengine wangefanya.''
Pili amesema hakuna aliyemshuku alikuwa
mwanamke.
''Nilijifanya kama nyani aina ya Gorilla''
alisema, Nilipigana, lugha yangu ilikuwa mbaya , nilibeba kisu kikubwa kama
Maasai.
Hakuna mtu alifahamu kwamba mimi ni mwanamke
kwa sababu kile nilichokuwa nikifanya nilikifanya kama mwanamume.''
Baada ya mwaka mmoja, alipata utajiri ,
alipopata mawe mawili makubwa ya Tanzanite. Kutokana na pesa alizozipata
alimjengea babake, mama na pacha wake nyumba mpya na akajinunulia vifaa zaidi na
akaanza kuajiri wachimba migodi kumfanyia kazi.
Na kujificha kwake kuliwashawishi kwamba
alichukua hatua zisizo za kawaida kwa utambulisho wake kujulikana.
Mwanamke mmoja aliripoti kwamba alikuwa
amebakwa na wachimba migodi Pili akiwa miongoni mwa washukiwa.
''Polisi walipokuja, wanaume waliotekeleza
ubakaji huo wakasema: 'Huyu ndio mwanamume aliyetekeleza hilo'' na nilipopelekwa
katika kituo cha polisi , Pili akasema alikuwa hana namna bali kutoboa siri
yake.''
''Aliwauliza polisi kumleta polisi mwanamke ili
amchunguze kwamba yeye hakutekeleza kitendo hicho na baadaye aliachiliwa huru.
Hata baada ya hilo wachimba migodi wenzake waliona vigumu kuamini walikuwa
wamedanganyika kwa siku nyingi''.
''Hawakuamini hata polisi waliposema kwamba
alikuwa mwanamke," alisema, ''haikuwa rahisi kwao kukubali hadi mwaka 2001
nilipoolewa na nikaanza familia.''
Kutafuta bwana wakati kila mtu amenizoea kama
mwanamume haikuwa rahisi, Pili alipata bwana na akafanikiwa.
Swali lililokuwa akilini mwake lilikuwa,'je ni
mwanamke kweli?'' anakumbuka. ''ilimchukua miaka mitano ndipo
aliponikaribia.''
Pili aliikuza taaluma yake na hivi leo
anamiliki kampuni yake ya migodi ambayo ameajiri wachimba migodi 70 , watatu
kati yao ni wanawake, lakini wanafanya kazi ya upishi.
Pili amesema licha ya kwamba kuna wanawake
wengi katika makampuni ya migodi kuliko wakati wake, hata leo ni wanawake
wachache wanaofanya kazi kwenye migodi hiyo.
''Wanawake wengine huyaosha mawe hayo , wengine
ni wakala na wengine ni wapishi'' , alisema, ''lakini hawaingii ndani ya migodi
, si rahisi kumpata mwanamke akifanya nilichofanya wakati wangu.''
Mafanikio ya pili yamemuezesha kuwalipia karo
watoto wa ndungu zake 30 na wajukuu. Licha ya hayo amesema hawezi kumrai mwanawe
kufuata nyayo zake.
''Najivunia kwa kile nilichokifanya, imenifanya
tajiri lakini ilikuwa vigumu kwangu'', amesema.
''Nataka kuhakikisha mtoto wangu ataenda shule
apate elimu na ataweza kujiendeleza kimaisha kwa njia tofauti mbali na
nilivyopitia.''
No comments