Mafanikio; Mambo ya msingi unayopaswa kujiambia mwenyewe kila wakati.
Haya ndiyo Mambo
matano unayopaswa kujiambia mwenyewe
kila siku.
Katika kitu ambacho kitakuwa na thamani kubwa katika maisha
yako, ni vile amabavyo utakuwa na uwezo wa kujinenea mambo chanya kila wakati.
Kwani watu wengi wamekuwa hawafanikiwa kwa sababu wamekuwa ni wau ambao
wanajikatisha tamaa tamaa wao wenyewe.
Hivyo ili kuondokana na thana hiyo haya ndiyo mambo ambayo
unatakiwa kujiambia mwenyewe mara kwa mara kila uianzapo siku yako.
1. Leo ni siku yangu ya kuweza kufanikiwa kwa kutenda kile
nilichokuwa nimekipanga jana.
2. Mimi bora hakuna wa kunikatisha tamaa, kwani hatima ya
maisha yanu ninayo mwenyewe.
3. Kwa haya nitakayotenda leo naamini mimi nitakuwa mshindi
kwani yatakwenda kubadilisha historia ya maisha yangu.
4. Mimi naweza, na nitafanya kwa ubora jambo hili kwani hakuna wa kunizua kuyapata mafanikio yangu.
5. Kwa hayo yote naamini ya kwamba mwenyezi Mungu atakuwa
nami katika kunisimamia hayo yote ambayo nityatenda siku ya leo.
Hayo ni baadhi ya maneno amabyo unapaswa kujiambia kila
wakati na kila siku unapoianza siku yako ya mapambono dhidi ya kuuaga umaskini.
Na ili hayo yote yakamilike unahitaji kuamini na kuwa chanya
kila wakati.
Ndimi afisa mipango Benson Chonya
bensonchonya23@gmail.com

No comments