Linah apiga dili la Diamond Platnumz
Wakati watoto wa mwanamuziki Diamond Platnumz
wakiwa mabalozi wa maduka ya nguo za watoto, mwanamuziki Linah Sanga
anayetarajia kujifungua hivi karibuni amepata ubalozi wa duka la nguo za
watoto.
Linah ambaye ni mwanamziki wa nyimbo za kizazi
kipya amepata dili hilo la kuwa balozi wa duka la nguo za watoto la Kids City
Shopping (KCS), zikiwa zimebaki wiki chache kabla ya kujifungua mtoto wake wa
kwanza.
Linah ambaye mapema wiki hii alitambulisha
herufi ya mwanzo ya jina la mtoto anayemtarajia baada ya kuweka picha ya
ujauzito kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika ‘Baby T on the
way’,anakuwa miongoni mwa mastaa ambao watoto wao wamepata bahati ya kuwa
mabalozi.
“Kwa mara ya kwanza nitazungumza na mashabiki
wangu mwishoni mwa wiki hii kwa niaba ya KCS ambao ni wauzaji wa bidhaa
mbalimbali za watoto na akinamama wajawazito,” amesema Linah.
Hivi karibuni Linah alizindua wimbo wake mpya
‘Upweke’ na kupita katika vituo mbalimbali vya redio, televisheni na magazeti
kwa ajili ya kuutangaza wimbo wake huo mpya.
Mwanadada huyo ambaye hivi karibuni alimtangaza
mpenzi wake anayetarajia kuwa baba wa mtoto wake aitwaye Shabani ambaye pia ni
bosi wake, Linah amedai kuwa anafuraha kuwa mjamzito kwa kuwa ni kitu ambacho
alikuwa akitamani kwa muda mrefu.
“Ninafuraha kubwa kwa sababu ni kitu ambacho
kama mwanamke nilikuwa nakitamani siku zote kwamba na mimi nije niitwe mama,
nafuraha nimepata mtu sahihi wa kuwa mzazi mwenzangu ambaye nitalea naye
watoto,”amesema.
Mzazi mwenzake ambaye pia ni mkurugenzi wa
Kampuni Drops Up Entertainment ambayo inamsimamia Linah, amesema wamejipanga
kuhakikisha Linah anafika mbali zaidi kimziki
No comments