Madam Flora: Tujifunze kuwa na maamuzi binafsi
Ikiwa leo ni mwezi mmoja na siku kadhaa toka msanii wa Injili Madam
Flora kufunga ndoa kwa mara ya pili na mume wake Daudi Kusekwa baada ya
kuachana na aliyekuwa mume wake Emmanuel Mbasha, Fora amefunguka na
kuwataka watu kuwa na maamuzi binafsi.
Msanii huyo amewataka watu kuwa na maamuzi binafsi kama wanataka kufikia
ndoto zao na kudai kuwa unaweza ukawa unamshirikisha mtu lakini mtu
huyo asiwe na nia njema na wewe hivyo anaweza kukushauri ndivyo sivyo.
"Jifunze kuwa na maamuzi yako binafsi, sio kila jambo lazima ushirikishe
watu ndipo ulifanyie maamwuzi kwani si kila unayemshirikisha anakuwazia
mema. Pokea ushauri vizuri kabisa lakini jifunze kuwa na maamuzi
binafsi ili kutimiza ndoto yako" alisema Madam Flora
No comments