Nikki wa Pili atangaza hali ya hatari kwa wasanii

Msanii kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili amesema muda wowote ataachia ngoma mbili mpya pamoja na video zake na kudai uji huo utakuwa habari mbaya kwa wasanii wengine.

Rapper huyo amesema amekuwa kimya kutokana na project nyingi za kundi kuingiliana lakini sasa hivi yupo tayari kuachia ngoma mpya. “Ngoma zote zimeshashutiwa, kinachojadiliwa ni tuachie ngoma zote kwa wakati mmoja au tuzipishanishe kwa wiki moja au mbili, bado tunaangalia,” Nikki ameiambia kipindi cha E Newz cha EATV.
“Na kitu kingine ni kwamba watu wanajua ujio wa Nikki wa Pili, flow mashairi, ubunifu. Ni habari mbaya kwa MC wengi, labda niseme Nikki is coming,” ameomgeza.
Hata hivyo Nimsanii huyo amesisitiza kila mtu ana nafasi yake katika muziki lakini yeye ni mtu ambaye analeta flow mpya kwa kila wimbo mpya, sound tofauti, na hajawahi kurudia sound, hivyo wimbo wake utakuwa hit ndani ya saa 24.

No comments

Powered by Blogger.