Umuhimu wa Kujiongeza katika maisha ya mafanikio.
Habari za muda huu
mpenzi msomaji wa mtandao huu wa shwari media, ni matumaini yetu mazima u
mzima wa afya tele na unaendelea vyma katika harakati zako za kuweza kulisukuma
gurudumu hili la maendeleo. Ni siku
nyingine tulivu ambayo sina budi nikukaribishe kwa moyo mkunjufu tuweze
kujifunza kwa pamoja.
Siku ya leo nataka
ttuzungumzie namna ambayo una uwezo mwingine wa kutenda jamno jingine ambalo
linaweza kukupa mafanikio makubwa kwa upande wako tofati na hilo ulitendalo
sasa. Unajua nataka tuzungumzie hili kwa sababu wetu wengi hawafahamu uwezo
mwingine walionao, ambao unaweza kuutumia ili uweze kukamilisha jambo jingine
ambalo Mwenyezi mungu kakujalia kiulitenda.
Watu wengi hudhani ya
kwamba hicho ambacho wanakifanya ndicho ambacho wamepangiwa kufanya. Kwa mfano
mtu ni mfanyabishara fulani, labda huenda mtu akawa amesomea kitu fulani, basi
baada kuweza kubobea katika kipengekle hicho, basi anaweka mipaka katika kitu hicho
pekee.
Ukweli haipo hivyo
hata chembe, kwani kila binadamu binadamu kaumbwa na uwezo mwingine wa kufanya vitu vingi
ambavyo vitaweza kumuinua kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ya
kimafanikio. Hata kanuni ya kufanya mazoezi ya mwili inasema ya kwamba huwezi
kutengeneza six park kwa kufanya mazoezi ya aina moja pekee kila wakati, bali
unaweza kutengeza six park kwa kufanya mazoezi ya aina tofauti tofauti.
Kwa muktadha huo kama kweli unataka kufanikiwa
zaidi ya hapo ulipo sasa, unachotakiwa kufanya ni kuweza kutambua uwezo
mwingine ambao mwenyezi Mungu kakuwekea ndani yako, ili uweze kujipatia mkate
wako wa kila siku.
Hata mwandishi mmoja
aitwaye Antony Robbison aliwahi kuandika ya kwamba “if you do what you have done you will get what you always gotten”
hii ikiwa na maana “kama utafanya mambo yaleyale ambayo umekuwa ukifanya siku zote, utapata yale yele ambayo
siku zote umeyapata”. Naomba urudie kusoma tena aya hii ili uielewe
vizuri.
Kwani aya hiyo ipo
wazi kabisa kama umezoea kufanya mambo yale yale kwa njia ile ile basi matokeo
yake, yatakuwa ni yaleyale. Hivyo ili uweze kupata matokeo ya iana tofauti na uliyoyazoea, unachotakiwa kufanya kubomoa
uzio wako wa kufikiri kwa kuanza kubadili ratiba ya kutenda mambo yako ya
msingi. Lakini pia ongeza uzio wa kufanya mambo yako kwani binafsi naamini una kitu kingine cha
kufanya zaidi ya hicho ambacho unakifanya.
Mwisho nimalizie
makala haya kwa kusema ukitaka kwenda mbali zaidi katika mambo yako ya msingi
acha kujenga uzio ambao utakufanya ushindwe kuona fursa nyingine, bali unachotakiwa kufanya ni kubomoa uzio huo
ili uweze kuona fursa mbalimbali ambazo zimejificha, kwani pindi unavyoacha
ukuta huo ni kule kutengeneza uwezo wako wa kulalamika, na mwisho wa siku
kuelekea jehenamu ya umasikini.
Narudia kwa kusema
tena pale unaposhindwa kujiongeza ni kutengeneza jehanamu ya umaskini. Usiogope
na kusema afisa mipango anakutisha hapana,
ila kazi yangu ni kukwambia
ukweli ambao upo wazi, kwani nafasi uliyonayo sasa unachotakiwa kufanya ni
kuwaza ni namna gani utaweza kufika mbali zaidi.
Kwani umuhimu wa
kujiongeza kunamsaidia mtu kuweza kuwa milango mingi ya kuweza kufanikiwa
zaidi. Pia faida nyingine ya kujiongeza humsaidia mtu kuweza mbunifu zaidi kwa
kile akifanyacho. Na ubunifu humsaidia mtu aweze kujilikana na ukijulikana ndo
mwanzo wa mafaniko yenyewe. Mpaka kufikia hapo sina la ziada naomba kazi ibaki
kuwa kwako kwa kuamua kwenda kuyatekeleza hayo ambayo nimekwambia. Asante.
Ni wako katika ujenzi
wa mafaniko; afisa mipango Benson Chonya
0757909942.
No comments